Kalunde Band Valentine's Special

Watu mbalimbali wako katika hekaheka ya kusherehekea siku ya wapendanao maarufu kama Valentine’s Day. Lakini KALUNDE BAND inajiunga katika sherehe hiyo ikiwa na sababu ya ziada kuserebuka na kuserebusha mashabiki wake katika siku hii kwa onesho maalumu  litalofanyika Alhamisi siku ya Valentine pale katika kiota cha maraha cha wapendanao cha Trinity maeneo ya  Oysterbay jijini Dar es salaam karibu na Ubalozi wa Uganda.

Onesho hilo litaanza  Saa 1:00  jioni na kuendelea hadi saa 6:00 usiku.

 Siku ya Valentine ni muhimu kwa Kalunde kwani ndiyo siku ambayo bandhii  ilianzishwa. Band ilianzishwa tarehe 14.02.2006.

 Kukupa burudani hiyo ya kuadhimisha siku ya wapendanao sambamba na HAPPY BIRTHDYA ya kutimiza miaka saba kamili ya KALUNDE BAND ni kundi zima la bendi hiyo kama ifuatavyo. 

Deo Mwanambilimbi - Rais wa Band - Muasisi wa Band.
 Debora Nyangi - Meneja - Muasisi
Bob Rudala - Kiongozi wa wanamuziki
Bony Kaprobo - Solo Guitar - Band Stage Leader
Shehe Mwakichui - Keyboard Player / Mwimbaji - Muasisi wa band
Edson Allen (Eddy) - Solo Guitar
Othman Amri Majuto - Bass Guitar #
Rajab Nyunyusa - Tumba Alfa - Drummer
Mackie Fanta - Mwimbaji
Devotha, Mwapwani Yahya, Shila, Amina, wote hawa ni waimbaji
 ENEO : TRINITY OYSTERBAY KARIBU NA UBALOZI WA UGANDA
 KIINGILIO: Tsh. 5,000.00
 GETINI : ZAWADI NI GLASS OF WINE AU SHAMPEIN
 MUDA: SAA 1:00 JIONI - SAA 6:00 USIKU
 PIA COUPLE ITAKAYOPENDEZA WATAPEWA ZAWADI MAALUM USIKU HUO.        
RAIS WA BENDI YA KALUNDE DEO MWANAMBILIMBI AKIONGOZA MASHAMBULIZI KATIKA MAONESHO MBALIMBALIxoxo
Missie Popular

0 comments:

Post a Comment