From the Familia Kitchen Party Gala Tour 2014,Dar es Salaam

The Dar es Salaam tour of Familia Kitchen Party gala, tooka place this weekend. It featured a red carpet event, talks by Aunt Sadaka, Mama Victor and Chris Mauki as well as a FREE chance for women to check their health (Cervical Cancer and Family Planning eduction)
The number of women that showed up was impressive...though not as many as I expected,I blame it on the rain :( ...Anyhow...there was also abundant entertainment from Shaa, Mwasiti and Khadija Kopa... As we all know that,this year's event was sponsored by Familia,let's see what Familia is all about.


 PSI/Tanzania ni Shirika lisilokuwa la kiserikali lililojikita katika kuboresha maisha ya watanzania  kwa kutoa elimu na huduma za afya pamoja na  kusambaza bidhaa za afya kote nchini. Katika kupambana na magonjwa sugu kama vile UKIMWI, Saratani ya mlango wa Kizazi, Malaria na vifo vya kina mama, PSI/ Tanzania hushirikiana na wizara ya afya kuhakikisha malengo ya millenia kwa upande wa afya yanatimia.



PSI/ Tanzania iliazisha huduma za afya kupita chapa (Brand) yake ya FAMILIA mwaka 2009 ikiwa na huduma za uzazi wa mpango na baadae mwaka 2013 huduma ziliongezeka zikiwemo afya ya watoto, huduma za mwanamke baada ya kuharibika kwa mimba na Saratani ya mlango wa kizazi. Familia hufikisha huduma hizi kwa jamii kwa kupitia wadau wake katika serikali na sekta binafsi za vituo za afya. Hivi sasa, Familia inafanya kazi na vituo vya afya binafsi visivyopungua 250 katika mikoa 13 ya Tanzania ikiwemo , Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Mara, Tanga, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya na Arusha



Katika harakati za kupunguza vifo vya kina mama, Kupitia chapa (brand) yake ya FAMILIA, PSI imeshirikiana na Women Footprints Initiative kuwaletea  Women in Balance “Familia Kitchen Party Gala”  ambayo imeshafanyika Dodoma na Mwanza ambapo wanawake zaidi ya 200 walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi na 9 kati yao walionekana kuwa na viashiria vya ugonjwa huu na waliweza kupatiwa matibabu ya awali papo hapo. Wikiendi hii, siku ya Jumapili sherehe hizi zitafanyika hapa  Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Sherehe hizi ambazo  kuhudhuriwa kwa wingi na akina mama zina kusudio la ziada la kuhakikisha kuwa pamoja na elimu ya ujasiriamali, saikolojia, na mahusiano, mwanamke anapata fursa ya kujifunza Kujitambua, Kujipenda na Kujithamini katika swala zima la Afya ya uzazi na Saratani  ya mlango wa  kizazi. 



Dhima ya ushirikiano huu ni kwa lengo la;
1.       Kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi,
2.       Kutoa elimu sahihi kuhusiana na uzazi wa mpango pamoja na afya ya kizazi,
3.       Kutoa huduma hizi wakati wa Shughuli hii.



Kampeni hii imejikita katika kutoa elimu sahihi ya uzazi wa mpango na saratani ya mlango wa kizazi  ambapo huduma hizi zitatolewa bure kabisa. Hapa nchini, Saratani ya mlango wa kizazi  sio tu Saratani inayoongoza katika vifo vya kina mama bali pia ni aina ya Saratani ambayo imekuwa ikikuwa kwa kasi na katika nchi hizi za Afrika Mashariki, Tanzania ina  mzigo mkubwa zaidi ya gonjwa hili ikisababisha vifo 37.5 katika ya wanawake 100,000. 




Pia tukiangalia vifo vya kina mama, vingi hutokea wakati wa uzazi, kwa maana hiyo swala la Uzazi wa mpango ni swala nyeti na la umuhimu katika kupunguza  vifo hivyo. Twakimu zinaonyesha kuwa, matumizi ya njia za uzazi wa mpango yamekuwa yakikuwa katika kasi ndogo ambapo twakimu zinaonyesha kuwa asilimia 27% tu ndio wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.  Jambo hili limepelekea vifo vya kinamama kupungua taratibu sana. Matumizi duni ya njia za uzazi wa mpango, yamepelekea wanamama wengi kuzaa mara kwa mara jambo ambalo linawapelekea kuzorota kwa afya zao na pia afya duni za watoto wanaowazaa na hata kupoteza maisha wakati wa uzazi .




FAMILIA imedhamiria kuhakikisha kuwa Wanawake/Wanamama wa Dar es Salaam wanapata ufahamu na elimu sahihi pamoja na kutoa mwongozo wa wapi pa kupata huduma hizi za uzazi wa mpango pamoja na upimaji na matibabu ya awali ya saratani  ya mlango wa kizazi. .... Familia: Huduma za afya zinazoaminika




Kwa Maelezo  Zaidi, Wasiliana na:

FAUZIYAT ABOOD
HEAD OF GOVERNMENT & MEDIA RELATIONS DEPARTMENT
Mobile:  + 255 754 281338
Email: fabood@psi.or.tz
www.psi.or.tz



xoxo
Missie Popular

0 comments:

Post a Comment