Usiku wa kilele cha tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2014 unatarajia
kufanyika Jumamosi Mei 3. Kwa kutambua kwamba sio wote watakaoweza kufuatilia
kupitia Televisheni kutokana na baadhi kuwa nje ya Tanzania, tukio hilo
linatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja mtandaoni ambapo watazamaji wataweza
kufuatilia kupitia simu au kompyuta zao katika BLOG HII.Link ya Kutazama itakua hewani Jumamosi kuanzia saa TISA mchana
Usiku wa tuzo unatarajiwa
kuanza saa moja jioni kwa Red Carpet
ambapo watangazaji Jokate Mwegelo, Millard Ayo na Salma Msangi watawahoji
mastaa mbalimbali watakaokuwa wakiwasili ukumbini na baadaye kuungana na Mtangazaji
wa EATV Sam Misago katika Social Media Lounge kuelezea yanayojiri katika tuzo
na kuhojiana na washindi.
xoxo
Missie Popular
0 comments:
Post a Comment