Baadhi ya madiva wa jiji la Mwanza wakiwa kwenye pozi la Red Carpet wakati wa Tamasha la “Trust Divas Only” ambalo lilifanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya akina dada na ni mahususi kwa ajili ya utoaji elimu ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae.
Msanii
wa Bongo fleva Vanessa Mdee, akipiga picha na baadhi ya mashabiki wake wakati
wa Tamasha la “Divas only” ambalo ni mahusisi kwa ajili ya kuwaelimisha madiva
mbalimbali kuhusu elimu ya afya ya uzazi. Tamasha hilo la mwisho lilifanyika
katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza baada ya kuzunguka katika
majiji ya Dodoma na Mbeya katika wiki zilizopita.
Shabiki wa Msanii Vanessa Mdee akiwa kwenye pozi
la Red Carpet wakati wa Tamasha la “Trust Divas Only” ambalo lilifanyika katika
hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo
ambalo ni maalum kwa ajili ya akina dada ni mahususi kwa ajili ya utoaji elimu
ya afya ya uzazi na maendeleo yao ya baadae
Wafanyakazi wa TRUST wanaohusika na mpango wa
kuelimisha wasichana juu ya elimu ya uzazi wakiwa jukwaani tayari kwa kufungua
Tamasha la “Divas Only” kwa kucheza muziki. Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi
wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Moja ya Madiva wa jiji la Mwanza akiimba accapela kwenye tamasha la “Trust
Divas only” lilofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza katika Ukumbi wa
Malaika Beach Resort. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya akina dada ambalo
lilitoa elimu ya afya ya uzazi kwa madiva wa jiji hilo.
Msanii wa Bongo fleva Vanessa Mdee akitumbuiza kwenye Tamasha la “Trust Divas
Only” lililofanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza
mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya kina dada na limekua
likitoa elimu juu ya afya ya uzazi na maendeleo ya baadae ya madiva hao tokea
uzinduzi wa mfululizo wa matamasha hayo jijini Dodoma wiki mbili zilizopita.
Mwanza
Tamasha la “Trust
Divas only” limefunga pazia lake rasmi usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa
Malaika Beach resort uliopo pembezoni mwa ziwa Victoria jijini Mwanza. Wakazi
na madiva wa mkoa huo walijitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha hilo la mwisho
na la aina yake lakini kikubwa zaidi kupata elimu na hamasa juu ya uzazi wa
mpango na mambo yanayowahusu wakina dada katika kupanga maendeleo yao ya
baadae.
Aliyelipamba Tamasha
hilo si mwingine bali ni diva wa nguvu na msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye
tokea awali amekua akishirikiana na Trust katika
mfululizo wa matamasha hayo yaliyoanza rasmi wiki mbili zilizopita jijini
Dodoma.
Mara baada
ya kupanda jukwaani na kuporomosha burudani ya nguvu Vanessa alionekana
kushangiliwa kila kona na madiva hao waliokuwa wakiimba sambamba na msanii huyo
ambae alifanikiwa kukata kiu ya madiva wengi wa mkoa huo waliojitokeza kwa
wingi kushuhudia burudani yake.
Mfululizo
wa matamasha hayo ya Trust ambayo ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango
zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa
kwa ajili ya wanawake yamefikia tamati baada ya kuzunguka kwa muda wa wiki tatu
kwenye miji mitatu tofauti ili kuhamasisha madiva mbalimbali wajipange kwa
ajili ya mafanikio yao ya baadae. Trust ipo katika kumsaidia diva wakati wote
wa safari hii.
“Ni
furaha yangu kubwa kuwa tumeweza kukamilisha zoezi hili kwa ufanisi mkubwa
tangu tulipozindua matamasha haya jijini Dodoma”… alisema Meneja Masoko wa
Trust Sialouise Shayo.
Bi.
Shayo aliongeza kuwa katika zoezi zima wamefanikiwa kuwafikia madiva lukuki
katika mikoa yote mitatu waliyoitembelea ambapo kwa
pamoja wameweza kufurahi, kuelimishana na kujifunza kutoka kwa wataalamu mambo
mbalimbali zikiwemo njia nyingi bora za uzazi wa mpango kama njia ya kitanzi
ambayo ni bora sana na ina ufanisi wa
zaidi ya asilimia 99.9.
Kama
wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, Tutafute kupitia ofisi
zetu zinazopatikana Dodoma, Mbeya na Mwanza au kwa kupitia tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo.
xoxo
Missie Popular
0 comments:
Post a Comment