Trust pamoja na Vanessa Mdee wazindua rasmi Tamasha la “Divas Only” mjini Dodoma...Mwanza na Mbeya kufuatia.

Mwishoni mwa wiki TRUST walizindua mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya "Divas Only" ambayo yalimshirikisha mwanadada na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee. Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa na wanawake kwa ajili ya wanawake. Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye. Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio; Trust iko hapa kukusaidia wakati wa safari hii. Tulifurahia muda tuliopata kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa Dodoma. Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika matamasha yetu mengine Mbeya Desemba 04 pale Sunset Hall, Soweto na Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tutafute kwenye ofisi zetu zilizopo Dodoma, Mbeya na Mwanza au kupitia tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!

 Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee (Wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na madansa wake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Trust “Divas Only” lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha hilo ni mahususi kwa utoaji elimu ya uzazi wa mpango kwa kina dada ambalo liliratibiwa na Shirika la DKT international.
 Msanii Vanessa Mdee (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la DKT International kabla ya kufungua rasmi Tamasha la Divas Only ambalo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Katikati) ni Meneja Masoko DKT International Sialouise Shayo.
 Kaimu meneja wa DKT International tawi la Dodoma Bi.Zena Mgoi akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa kina dada waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha la “Divas Only” ambalo lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
 Vanesa Mdee akitumbuiza katika tamasha la kutoa elimu ya uzazi wa mpango lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha lililopewa jina la “Divas Only Concert” lilifanyika katika ukumbi wa Royal Village na kuratibiwa na Shirika lisilokua la kiserikali DKT International.


xoxo
Missie Popular

0 comments:

Post a Comment