Baadhi
ya akina dada waliohudhuria burudani iliyotolewa na mwanamuziki Vanessa Mdee
jijini Mbeya kwenye hamasa ya matumizi ya uzazi wa mpango iliyodhaminiwa na
chapa ya Trust toka shirika lisilokuwa la kiserikali la DKT International. Tamasha
hilo lillilopewa jina la “Divas Only Concert” lilifanyika katika ukumbi wa
Mtenda Sunset-Soweto jijjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Msanii
Vanessa Mdee akitoa burudani kwa madiva wa jiji la Mbeya wakati wa Tamasha la
Trust “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika jijini humo katika ukumbi wa
Mtenda Sunset uliopo Soweto lengo la Tamasha likiwa ni kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa akina dada
na mama wa jiji hilo.
Msanii
Vanessa Mdee (katikati) akiwa pamoja na wanenguaji wake katika Tamasha la
“Divas Only Concert” lililofanyika katika ukumbi wa Mtenda Sunset-Soweto jijini
Mbeya mwishoni mwa wiki. Msanii huyo aliporomosha burudani ya nguvu kwa madiva
lukuki waliofika kushuhudia tamasha hilo ambalo lililoandaliwa na chapa ya TRUST
toka shirika lisilokua la kiserikali la DKT lengo la Tamasha likiwa ni kuwahamasiha
kuamka kifikra na kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wasichana na kina mama wa
jiji hilo.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee (Katikati) akiwajibika jukwaani mbele ya
umati wa akina dada waliojitokeza kwenye Tamasha la “Divas Only Concert” ambalo
lilifanyika katika ukumbi wa Mtenda, Sunset-Soweto jijini Mbeya. burudani hiyo ya
nguvu iliandaliwa na chapa ya Trust toka shirika lisilokuwa la kiserikali la
DKT International ambalo liliwakutanisha madiva kutoka sehemu mbalimbali wengi
wao wakiwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu
juu ya uzazi wa mpango.
Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ujio wake jijini Mbeya na mtazamo wake kwa akina dada juu ya uzazi wa mpango mara baada ya kumaliza kutumbuiza katika Tamasha lililopewa jina la “Divas Only Concert” ambalo lilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Mbeya Desemba 2015
TRUST imeendelea
kuzikonga nyoyo za mashabiki wake hususani wakina dada katika mfululizo wa matamasha
ya kusisimua ya “Divas Only” ambapo kwa wikiendi hii ilikua ni zamu ya jiji la
Mbeya baada ya Tamasha hilo kuzinduliwa rasmi jijini Dodoma mwishoni mwa wiki
iliyopita. Kama ilivyo ada Tamasha hilo humshirikisha Diva wa nguvu na msanii
wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee ambaye alizikonga nyoyo za mashabiki
wake vilivyo. Tamasha hilo liliwavutia madiva kibao kutoka maeneo ya karibu
pamoja na vyuo mbalimbali vya jijini Mbeya kama TECU, Mzumbe, CBE na TIA ambapo
kiingilio cha Tamasha hilo kilipangwa kuwa Tsh. 10,000/= tu. Trust ni chapa ya
njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za
maisha na urembo zinazotengenezwa kwa ajili ya wanawake. Trust ipo ili
kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye. Madiva wa Trust wanataka
kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio; Trust ipo hapa kukusaidia
wakati wa safari hii. “Kwa mara nyingine ilikuwa ni fursa nzuri ya kufurahi kwa
muda tuliopata wa kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa jijini Mbeya na
kufurahi na kuelimishana, tumejifunza kutoka kwa wataalamu mambo mengi na njia nyingi bora, kwamfano njia ya Kitanzi ni bora sana ina ufanisi wa
zaidi ya asilimia 99.9 na pia ni bora sana kwakua aina nyingi hazina
vichocheo ”…alisema Sialouise Shayo
Meneja Masoko Trust. Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu
nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika Tamasha
letu lingine jijini Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tutafute
kupitia ofisi zetu zinazopatikana Dodoma, Mbeya na Mwanza au kwa kupitia tovuti
yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!xoxo
Missie Popular
0 comments:
Post a Comment