Kudos to Blogger Othman Michuzi

Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a "Mzee wa Mtaa kwa Mtaa" wa Kampuni ya Michuzi Media Group juzi kati alitinga ndani ya Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,zilizokuwa zikitolewa katika ukumbi wa maraha na burudani pale Mlimani City,Jijini Dar.

Alichokifanya mwanalibeneke huyo Othman Michuzi kwa kutumia kamera yake au Jicho Kubwa lionalo mbali,ni kurekodi matukio mbali mbali ya usiku huo zikiwemo video za matukio,ambapo video hizo zinawezekana zikawa ndio tiketi ya kuupeperusha muziki wa Tanzania katika masoko ya kimataifa, labda wengi walistushwa na kiwango cha juu cha kimataifa katika video hii https://www.youtube.com/watch?v=ZDcmpDoZQZM

Wataalamu wa masoko wa kimataifa waliotazama video hiyo katika Youtube,wameshauri kuwa itakuwa jambo la busara kwa Kampuni ya Michuzi Media Group, Kuhifadhi haki yake katika video hizo, na mameneja wa wasanii au bendi wakae meza moja na menejmenti ya Michuzi Media Group,ili wakubaliane kutumia Bidhaa hiyo kuwa Demo ya kuwapromoti wasanii au bendi zao Duniani.

Kuzitumia bila ya ridhaa ya aliepiga video hizo ni kinyume cha sheria. Kukopi na kupesti bila ya Idhini au ridhaa ya walipiga video hiyo ni kuvunja sheria na heshima.

ni Ushauri tu, lakini Hongera nyingi sana sana kwa Mpiganaji Othman Michuzi kutoka kwa wadau wa ughaibuni,kwani Kazi aliyoifanya imeipeperusha vyema Bongo yetu Kimataifa endelea kwa kasi hiyo hiyo https://www.youtube.com/watch?v=lZYxySYLmI

Unaweza tembelea libeneke lake kwenye link hiyo http://www.othmanmichuzi.blogspot.com
Pia unaweza tembelea ukurasa wake wa youtube kwa link hii https://www.youtube.com/user/Michuzijr2?feature=watch ili kuona video mbali mbali.

Mdau Msema Kweli
Ughaibuni.

0 comments:

Post a Comment