The number of women that showed up was impressive...though not as many as I expected,I blame it on the rain :( ...Anyhow...there was also abundant entertainment from Shaa, Mwasiti and Khadija Kopa... As we all know that,this year's event was sponsored by Familia,let's see what Familia is all about.
PSI/Tanzania ni Shirika lisilokuwa la kiserikali
lililojikita katika kuboresha maisha ya watanzania kwa kutoa elimu na huduma za afya pamoja
na kusambaza bidhaa za afya kote nchini.
Katika kupambana na magonjwa sugu kama vile UKIMWI, Saratani ya mlango wa
Kizazi, Malaria na vifo vya kina mama, PSI/ Tanzania hushirikiana na wizara ya
afya kuhakikisha malengo ya millenia kwa upande wa afya yanatimia.
PSI/ Tanzania
iliazisha huduma za afya kupita chapa (Brand)
yake ya FAMILIA mwaka 2009 ikiwa na huduma za uzazi wa mpango na baadae mwaka 2013 huduma
ziliongezeka zikiwemo afya ya watoto, huduma za mwanamke baada ya kuharibika
kwa mimba na Saratani ya mlango wa kizazi. Familia hufikisha huduma hizi kwa
jamii kwa kupitia wadau wake katika serikali na sekta binafsi za vituo za afya.
Hivi sasa, Familia inafanya kazi na vituo vya afya binafsi visivyopungua 250
katika mikoa 13 ya Tanzania ikiwemo , Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma,
Mwanza, Mara, Tanga, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya na Arusha
Katika harakati
za kupunguza vifo vya kina mama, Kupitia chapa (brand) yake ya FAMILIA, PSI
imeshirikiana na Women Footprints Initiative kuwaletea Women in Balance “Familia Kitchen Party Gala”
ambayo imeshafanyika Dodoma na Mwanza
ambapo wanawake zaidi ya 200 walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya mlango wa
kizazi na 9 kati yao walionekana kuwa na viashiria vya ugonjwa huu na waliweza
kupatiwa matibabu ya awali papo hapo. Wikiendi hii, siku ya Jumapili sherehe
hizi zitafanyika hapa Dar es Salaam
katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Sherehe hizi ambazo kuhudhuriwa kwa wingi na akina mama zina kusudio
la ziada la kuhakikisha kuwa pamoja na elimu ya ujasiriamali, saikolojia, na mahusiano,
mwanamke anapata fursa ya kujifunza Kujitambua, Kujipenda na Kujithamini katika
swala zima la Afya ya uzazi na Saratani ya mlango wa kizazi.
Dhima ya
ushirikiano huu ni kwa lengo la;
1. Kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo
na uzazi,
2. Kutoa elimu sahihi kuhusiana na uzazi wa
mpango pamoja na afya ya kizazi,
3. Kutoa huduma hizi wakati wa Shughuli hii.
Kampeni hii imejikita
katika kutoa elimu sahihi ya uzazi wa mpango na saratani ya mlango wa kizazi ambapo huduma hizi zitatolewa bure kabisa. Hapa nchini, Saratani
ya mlango wa kizazi sio tu Saratani
inayoongoza katika vifo vya kina mama bali pia ni aina ya Saratani ambayo
imekuwa ikikuwa kwa kasi na katika nchi hizi za Afrika Mashariki, Tanzania
ina mzigo mkubwa zaidi ya gonjwa hili
ikisababisha vifo 37.5 katika ya wanawake 100,000.
Pia tukiangalia vifo vya kina mama, vingi hutokea wakati wa uzazi, kwa maana hiyo swala la Uzazi wa mpango ni swala nyeti na la umuhimu katika kupunguza vifo hivyo. Twakimu zinaonyesha kuwa, matumizi ya njia za uzazi wa mpango yamekuwa yakikuwa katika kasi ndogo ambapo twakimu zinaonyesha kuwa asilimia 27% tu ndio wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Jambo hili limepelekea vifo vya kinamama kupungua taratibu sana. Matumizi duni ya njia za uzazi wa mpango, yamepelekea wanamama wengi kuzaa mara kwa mara jambo ambalo linawapelekea kuzorota kwa afya zao na pia afya duni za watoto wanaowazaa na hata kupoteza maisha wakati wa uzazi .
FAMILIA imedhamiria kuhakikisha kuwa Wanawake/Wanamama
wa Dar es Salaam wanapata ufahamu na elimu sahihi pamoja na kutoa mwongozo wa
wapi pa kupata huduma hizi za uzazi wa mpango pamoja na upimaji na matibabu ya
awali ya saratani ya mlango wa kizazi. .... Familia:
Huduma za afya zinazoaminika”
Kwa Maelezo
Zaidi, Wasiliana na:
FAUZIYAT ABOOD
HEAD OF GOVERNMENT & MEDIA RELATIONS DEPARTMENT
Mobile: + 255 754 281338
Email: fabood@psi.or.tz
www.psi.or.tz
xoxo
Missie Popular
0 comments:
Post a Comment