Kilimanjaro Music Awards Kuonyeshwa Mtandaoni


Usiku wa kilele cha tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2014 unatarajia kufanyika Jumamosi Mei 3. Kwa kutambua kwamba sio wote watakaoweza kufuatilia kupitia Televisheni kutokana na baadhi kuwa nje ya Tanzania, tukio hilo linatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja mtandaoni ambapo watazamaji wataweza kufuatilia kupitia simu au kompyuta zao katika BLOG HII.Link ya Kutazama itakua hewani Jumamosi kuanzia saa TISA mchana 

Usiku wa tuzo unatarajiwa kuanza saa moja jioni kwa  Red Carpet ambapo watangazaji Jokate Mwegelo, Millard Ayo na Salma Msangi watawahoji mastaa mbalimbali watakaokuwa wakiwasili ukumbini na baadaye kuungana na Mtangazaji wa EATV Sam Misago katika Social Media Lounge kuelezea yanayojiri katika tuzo na kuhojiana na washindi.


xoxo
Missie Popular

0 comments:

Post a Comment