Na Evance Ng'ingo
MWANAMITINDO wa kimataifa afanyaye shughuli zake
nchini Marekani, Flaviana Matata madarasa mawili ya shule za msingi iliyopo
katika kijiji cha Msinune kilichopo kata ya Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani.
Flaviana alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na
wanakijiji wa Msinune mwaka 2014 wakati alipoenda kuwasaidia wanafunzi mabegi ya
shule, walimpatia jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja
na kumalizia ujenzi wa darasa.
Tangia alipopewa majukumu hayo alianza kwa ujenzi wa
vyoo vya walimu na wanafunzi, na juzi alienda kukabidhi jengo la madarasa,
darasa la saba na la sita pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Flaviana
alisema, tangia alipopewa jukumu la ulezi wa shule hiyo amekuwa akihangaika
huku na kule kupata fedha za kutatua kero za shule hiyo.
Alisema, kwa kufanikiwa kukabidhi jengo hio la
madarasa anaona kuwa ameshiriki kikamilifu katika kutekeleza jukumu lake kama
mwanajamii la kusaidia maendeleo ya elimu kwa jamii iliyokuwa na uhitaji
mkubwa.
Alisema" sisi kama vijana kama watanzania tunalo
jukumu la kujitokeza na kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine muhimu nchini
kwa kuwa hili sio jukumu la serikali peke yake, sasa nimeshatengeneza vyoo vya
walimu na wanafunzi na leo nakabidhi darasa"
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Alex
Lugaigalila alisema ujenzi wa darasa huo utawaongezea ufanisi wanafunzi katika
masomo yao huku akibainisha wazi ushiriki wa Flaviana kwenye maendeleo ya shule
hiyo umeongeza hamasa ya wanafunzi kusoma.
Kwa upande wake Afisa wa elimu wa Kata hiyo,Blasius
Alphonce alisema kwa ujenzi wa jengo hilo, Flaviana amesaidia jitihada za serikali
katika kuendeleza elimu kwenye kata hiyo yenye vijiji vitano.
Jengo hilo la darasa lililojengwa lina vyumba viwili
vikubwa vilivyoezekwa kwa bati huku likuwa na madirisha makubwa yanayowezesha
kupitisha hewa na chumba cha mwalimu mkuu.
0 comments:
Post a Comment